Serikali imeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara nchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji alipokutana wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuwasikiliza pamoja na kutatua changamoto zinawazowakabili.

Dk. Kijaji amesema kuwa tangu kuanza kutekelezwa kwa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara hapa nchini (Blue Print), Serikali imefanikiwa kuondoa kodi, tozo na ushuru mbalimbali 374 kati ya 380.

β€œTulianza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara mwaka 2019 na tulitamani kuondoa kodi, tozo pamoja na ushuru mbalimbali zilizokuwa zikilalamikiwa na wafanyabiashara nchini ambazo zilikuwa 380 kwa miaka Mitano.

Lakini leo tuko mwaka wa Nne tunatekeleza na tumeshaondoa kodi, tozo na ushuru 374 zimebaki Sita tuu na Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuzimaliza changamoto hizi zote lengo likiwa ni kuhakikisha mnafanya biashara katika mazingira mazuri na wawekezaji wanawekeza katika mazingira mazuri na yanayoibuka tunayabeba na kuendelea kushughulika nayo,” amesema Waziri Kijaji.

Dk. Kijaji pia ameagiza kitabu kinachoainisha kodi hizo zilizoondolewa kichapishwe ndani ya wiki moja na kifikishwe kwa Wakuu wa Mikoa ili wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali wajue kodi zipi zilizoondolewa kupunguza migogoro kati ya wafanyabishara na serikali.

Follow us on:
FACEBOOK;
SpotiLeo:
HabariLeo:
DailyNews:

INSTAGRAM;
HabariLeo:
SpotiLeo:

TWITTER;
Twitter HabariLeo:

The team at Kodi Fire IPTV strongly suggests that you use a VPN at all times.
Be it for browsing, watching Kodi, watching IPTV or anything else – the one that we recommend is Hidden Router. They provide you with very fast speeds, that can reach over 400Mbps, and their VPN service is as low as $6 per month (when paid for 2 years)!
Grab your own Hidden Router and regain your online privacy now!

1 COMMENT